f


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Saturday, September 18, 2010

NEWS IN FULL

MISS EARTH 2010 ROSE SHAYO KWENDA VIETNAM


MWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Miss Earth 2010, Rose Shayo aliondoka nchini jana kwenda Vietnam huku akiwa na matumaini makubwa ya kufanya vyema katika mashindano hayo.
Akizungumza kabla ya kuondoka, Rose alisema kuwa amejiandaa viliyvyo chini ya muandaaji ake, Maria Sarungi wa Compass Communications and bila shaka atafanya vyema katika mashindano hayo.
Rose amesema kuwa haendi kuwa msindikizaji katika mashindano hayo na atafanya kila aliwezalo ili kufanya vyema kama ilivyokuwa kwa Miriam Odemba mwaka 2008 nchini Philippines.
“Najua kuna kushinda na kushindwa, mimi sitarajii kushindwa kutokana na maandalizi yangu, nawaomba Watanzania wanipe sapoti kubwa wakati wote nikiwa kambini na siku ya mashindano,” alisema Rose.
Maria alisema kuwa, alisema mrembo huyo amejiandaa vizuri kwakuwa mashindano ya kumsaka mrembo huyo yalifanyika mapema mwaka huu.
“Mashindano ya kumsaka mrembo huyu yalifanyika tangu mwezi wan nne mwaka huu kutokana na hali hiyo alipata muda mwingi wakujiaandaa hali inayomuweka ka

DESIGNER'S KUTOKA NCHIMBALIMBALI

Wakiwa wamepozi katika picha ya pamoja.
Jukwaa la tatu la Swahili fashion Week linaanza leo katika viwanja vya karimjee jijini Dar es salaam na kudumu kwa muda wa siku tatu hadi tarehe 6 ya mwezi wa November 2010.
Katika jukwaa la mwaka huu jumla ya wabunifu 24 kutoka nchi za Afrika hasa zile zinazozungumza lugha ya Kiswahili wamejiandaa vya kutosha katika kuonesha kazi zenye viwango vya kimataifa.
“Tunashukuru kwani mipango yote inakwend kama tulivyopanga na tayari wabunifu wote wamefika kwa ajili ya shoo kabambe ambapo itakuwa na tofauti kubwa kulinganisha na zile zilizopita. Tayari wabunifu wote 24 kutoka Tanzania na nchi za Pan Afrika wapo tayari kwa shoo ya mwaka, inayoandaliwa nyumbani mwa Swahili Fashion Week.” Alisema Mustafa Hassanali muandaaji wa Swahili Fashion Week
“Kwa mara nyingine tena tupo na Swahili Fashion Week 2010, na kusaidia kukuza Sanaa ya ubunifu wa mavazi hapa nchini, pamoja na kuwakaribisha wageni wetu ambao ni wabunifu wa kimataifa. Southern Sun inajivunia kutokana na mchango wake inayotoa kwa Sanaa ya ubunifu wa mavazi Afrika na hii intupa fursa ya kuendelea kwa njia mbalimbali.” Alisema meneja mkuu wa southern sun Hotel Ndugu Adam fuller
Southern Sun hotel imekuwa nyumba ya Swahili Fashion Week toka mwaka 2009.
Swahili Fashion Week inafanyika kwa mwaka watatu sasa na itawashirikisha wabunifu 24 ambapo kwa mujibu wa ratiba, siku ya kwanza shoo itapambwa na Manju Msita (Tanzania),Sonu Sharma (Kenya),Shelina Ebrahim (Tanzania/Canada),United Against Malaria (Tanzania Various),Farha Sultan (Tanzania),Tanzania Mitindo House (Tanzania - Various), KemiKalikawe (Tanzania) na Asia Idarous (Tanzania)
Kwa upande wa tarehe tano, siku ya ijumaa mwanamitindo kutoka Tanzania Jamila Vera Swai tfungua pazia akifuatiwa na Marinella Rodriguez (Mozambique),Stella Atal (Uganda),Kooroo (Kenya),Zamda George (Tanzania),Mafi Designs (Ethiopia),Moo Cow (Kenya),Robi Morro (Tanzania),Made by Africa (Tanzania) na Asos Africa (UK)
Tarehe sita November siku ya mwisho ya jukwaa la Swahili Fashion Week, wabunifu wtakoonesha kazi zao ni pamoj na wabunifu wanane wanaochipukia waliofanikiwa kuingia fainali kupitia shindano la wabunifu wanaochipukia, Emerging Designers Competition (Tanzania - Various),Gabriel Mollel (Tanzania),Khadija Mwanamboka (Tanzania),KikoRomeo (Kenya), John Kaveke (Kenya), Chichia London (Tanzania/UK), Ailinda Sawe (Tanzania)
“ Pamoja na kuwakaribisha wageni wetu ambao ni wabinifu wa mavazi , pia Southern itatoa zawadi kwa gauni bora katika Swahili Fashion Week kwa huu , lengo ni kusaidia kukuza Sanaa ya ubunifu wa mavazi” Aliongeza Saphia Ngalapi, Swahili Fashion Week PR manager


BENJAMIN KUTOA SINGLE YAKE MPYA YA MY FRIEND
Katika wimbo huo benja amejaribu kuzungumzia maisha halisi amboyo baadhi ya marafiki huyafanya kwa marafikizao na kusahau misaada au fadhila walizopewa na marafikizao.

KANUMBA KUVUMBUA KIPAJICHA MAGESE KWENYE FILAMU YA UNCLE JJ

Kanumba na Magese Tukiwa location tukijiandaa na sini
Mdau wa mitindo na urembo mr. magse amepata shavu toka kwa swaiba wake wa siku nyingi The Greatsteve Kanumba ''moviez king' kwa kuahidi kufanya kila liwezekanalo kumfikisha swaiba
wake magese katika anga za filamu kimataifa.